Barabara ya Tanzania Kwenda Damascus
Mwijage, Ludovick Simon Baada ya Vita Vikuu kumalizika 1918 Ujerumani iliachia miliki zake za nje, ikiwemo miliki yake ya Afrika Mashariki, kwa umoja wa mataifa makuu na mamlaka-shiriki (Principal Allied and Associated Powers) yaliyoshinda vita. Kutokana na mabadiliko hayo, Uingereza ilikubali wajibu wa kimataifa wa kusimamia sehemu kubwa ya miliki ya Kijerumani ya Afrika Mashariki, ambayo baadaye iliitwa Jimbo la Tanganyika (Tanganyika Territory), hadi hapo wenyeji ...