Karamu Mbinguni
Kimunyi, Njiru Kutokana na sifa zao njema kwake Mwenyezi Mungu, ndege wamepata mwaliko wa kutalii mbinguni. Wamepewa uwezo wa kuyabadilisha maumbile yao vile wanavyotaka. Katika kufanya hivi, wengine kama Bundi wanaongozwa na nia mbaya. Mzee Kobe naye anadanganya kuwa ukoo wake ulitokana na ndege. Kwa wale wenye nia safi, karamu ya mbinguni inaishia kuwa furaha isiyo kimo. Wenye nia mbaya nao wanaupata mshahara wa vitendo vyao. Chongameno ni kijana mchungaji...